slider

Recent

Designed by mwarabusope. Powered by Blogger.

About Me

Total Pageviews

Search This Blog

Popular Posts

Navigation

Hii ndiyo sababu betri ya laptop yako inaisha chaji haraka






Ni nini kinasababisha betri ya laptop kuisha haraka? ukijibu mwanga wa kioo utakuwa sahihi kwa asilimia kubwa.

Kitu kikubwa kinachomaliza betri ni kioo cha laptop. Umeme mwingi sana unatumika kwenye taa zilizopo nyuma ya kioo ambazo zinamulika kioo ili picha ionekane kwenye laptop yako.

Njia pekee ya kuifanya betri ikae muda mrefu ni kupunguza mwanga wa kioo. kwenye laptop ya Window 10 au Apple MacBook, unaweza ukapunguza mwanga kwa kutumia keyboard yako, ila kuna baadhi ya njia zingine rahisi ambazo unaweza ukazitumia.



Badilisha mipangilio(settings) ya kioo chako

Badilisha mipangilio ya mwanga kwenye Mac OS X

Fungua System Preferences kisha bonyeza Display. Kwenye Display tab, utaona slider kwa ajili ya Brightness. Ivute hiyoo slider kuelekea kushoto ili kupunguza mwanga. Hii siyo tu inapunguza mwanga na kusaidia betri yako ikae muda mrefu, pia itasaidia kwa afya ya macho yako labda kama utakaa kwenye mwanga wa jua ambapo mwanga wa kioo chako lazima uwe mkubwa ili kuweza kuona unachokifanya.



   

Windows 10 
Kama unahofia na kuisha haraka kwa betri ya laptop yako inayotumia Windows 10, nenda kwenye Control Panel > Hardware and Sound > Power Options halafu hakikisha unachagua mpango wa Balanced au Power Saver. Tumia mpango wa High performance pale unapokuwa umechomeka laptop yako kwenye moto au unataka kuongeza nguvu ya ufanyaji kazi kulingana na App unayotumia au unacheza game.



                                            Game zinahitaji mpango wa High Performance ili kucheza vizuri

Ukiwa na Window 10, pia kuna mipangilio mingine ya kuhifadhi betri na kurekebisha kioo vizuri ili kulipa betri muda mwingi zaidi wakati unatumia laptop yako, kwenye Settings button ambayo ipo kwenye start screen ya Windows 10, gusa System. kisha gusa tena Display iliyopo kwenye menu ya kushoto utaona slider iliyoandikwa Adjust brightness level ya kupunguza na kuongeza mwanga.




Kisha, hapo kwenye menu ya kushoto gusa Battery Saver. kisha gusa hiyo batani chini ya maneno yaliyo andikwa Battery saver is currently kama hiyo batani ni ya kijivu, chomoa chaja ya laptop yako hiyo swichi itabonyezeka. Kipengele hicho cha Battery saver ni kipya kwenye Windows 10 ambapo kinapunguza app zinazofanya kazi kwa siri na kuifanya laptop iwe nyepesi zaidi bila mizigo ili iweze kukaa na chaji kwa muda mrefu.



Hii ndiyo sababu betri ya laptop yako inaisha chaji haraka


Kawaida, Laptop inajiweka katika Battery saver pale chaji inapokuwa imepungua mpaka asilimia 20. Gusa Battery saver settings kuongeza asilimia hii. Pia kwenye ukurasa huo huo unaweza ukatia sahihi kwenye kiboxi kilichoandikwa Lower screen brightness while in battery saver ili kuongeza zaidi muda wa betri yako.

Hii ndiyo sababu betri ya laptop yako inaisha chaji haraka
Unaweza pia kuongeza asilimia kutoka 20 hadi unayotaka


Mwisho kabisa, gusa kwenye Power & sleep hapo kwenye menu ya kushoto halafu weka muda ambao laptop yako itazima kioo chako na kuilaza PC yako ili kupunguza upotevu wa betri usio na sababu wakati laptop yako ikiwa haitumiki.

Hii ndiyo sababu betri ya laptop yako inaisha chaji haraka
Weka muda ambao laptop yako itajizima pindi itakapo kuwa haitumiki



Usisahau taa za kwenye keyboard

Kama ilivyo kwa taa zilizo nyuma ya kioo cha laptop yako, umeme unaotumika kwenye taa za keyboard nao pia unaweza ukawa ni kinyonyeo kikubwa cha betri yako. Kwanza, hakikisha kuzima taa za kwenye keyboard yako kama hauzitumii. Pili, mifumo yote inayoendesha PC na Apple (Windows 10 na OS X) ina sehemu za mipangilio ya kuzima taa za keyboard kama laptop ikikaa bila kutumika kwa muda ambao utachagua wewe. Ila mpangilio huu unategemea na brand ya laptop yako yaweza ikawa Hp, Dell au Lenovo kila moja ina aina yake ya mipangilio jinsi ya kupunguza mwanga kwenye Windows 10, ila kwenye Apple OS X utaikuta kwenye System Preferences > Keyboard

Hii ndiyo sababu betri ya laptop yako inaisha chaji haraka
Badilisha mipangilio ya taa za kwenye keyboard
Share
Banner

Mwarabusopeblog

Post A Comment:

0 comments: